18 Aprili 2025 - 20:50
Source: Parstoday
Ayatullah Khatami: Iran haishurutishwi wala haisalimu amri

Khatibu wa Swala ya leo ya Ijumaa katika jiji la Tehran ameashiria mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani kuhusu suala la nyuklia na kuondolewa vikwazo na akasema: "Katika mazungumzo hayo, tunapasa kuwa makini na tusimtegemee yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, tusichoke kupambana, na tusifungamanisha hatima yetu na mazungumzo."

Akizungumza katika hotuba yake ya kwanza ya Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema: Kwa kuzingatia kuwa hivi sasa, mjadala unaoendelea duniani na Iran ni mazungumzo ya Iran na Marekani;  kwa hiyo tunapasa kuzingatia mambo kadhaa katika suala la mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja.

Amesema miongoni mwa mambo hayo ni kwamba tusiweke tumaini letu kwa yeyote zaidi ya Mwenyezi Mungu. "Tunapaswa kumtegemea Mungu peke yake katika kila jambo. Maadui wanapasa kujua kwamba taifa la Iran haliwezi kuwekewa vikwazo wala kusalimu amri."

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema mazungumzo hayo yanahusu suala la nyuklia tu na hatutafanya mazungumzo juu ya maswala mengine.

Ayatullah Khatami: Iran haishurutishwi wala haisalimu amri

Ameongeza kuwa: "Sababu ya kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani ni kwamba hatuna imani na upande wa pili na wanakaa katika kumbi mbili tofauti na kubadilishana ujumbe."

Ayatullah Khatami amesema: Trump amesema mara kadhaa kwamba machaguo yote yako mezani (dhidi ya Iran); na sisi tunasema: "Machaguo yetu pia yako kwenye meza. Chaguo letu la kwanza ni kwamba Iran haikubali kutwishwa wala haitasalimu amri. Ikiwa utachukua hatua yoyote dhidi yetu, bila shaka na hakika tutalipiza kisasi."

Katika hotuba yake pili, Ayatullah Khatami amesema: Imam Ali bin Abi Twalib (a.s) amesema: Hatukuumbwa kwa ajili ya dunia. Tumekuja kutahiniwa ili Mungu akipenda tuweze kujinunulia Akhera na kufaulu vizuri mtihani huo. Huu ndio wito wa Uchamungu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha